angalia picha za yanga sport club vs azam fc

Yanga sport club yaimaliza AZAM FC1-0

MECHI ya Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda Azam bao 1-0.
Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.
Uwanja sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. [[PASTING TABLES IS NOT SUPPORTED]]13,341,716.86, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh. 13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.
Katika mchezo huo, bao pekee la kiungo Salum Abdul Telela ndilo lililoipa Yanga SC ushindi huo.
Mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Yanga ilipata bao hilo mapema tu dakika ya pili, mfungaji kiungo Salum Abdula Telela aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbangu.
Baada ya bao hilo, Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Azam na kipa Aishi Manula alifanya kazi ya ziada kuokoa.
Dakika ya 11, Yanga ilipata pigo baada ya beki wake Kevin Yondan kuumia kufuatia kugongana na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Aedebayor’. Yondan alitibiwa kwa dakika nne, lakini akashindwa kurejea uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na Mbuyu Twite dakika ya 15.
Dakika tano baadaye Yanga ikapata pigo lingine baada ya kipa wake, Ally Mustafa ‘Barthez’ kuumia kufuatia kugongana na Kipre Tchetche.
Barthez ‘alijitoa muhanga’ kuutokea mpira miguuni mwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast baada ya kuwatoka mabeki wake, Juma Abdul na Nadir Haroub ‘Cannavaro’- hivyo kugongwa kifuani na mguu wa Kipre.
Barthez alitibiwa kwa dakika nne kabla ya kumpisha Deo Munishi ‘Dida’.  Azam waliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Yanga na dakika ya 30 Kipre Tchetche alifumua shuti kali likagonga mwamba na kutoka nje akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Bocco.   
Aishi Manula alikuwa majaribuni tena dakika ya 30 baada ya krosi maridadi ya Simon Msuva kumponyoka kabla ya kuondoshwa hatarini na Erasto Nyoni.
Dakika ya 38 Dida alidaka shuti kali la mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita Kipre Tchetche kutoka umbali wa mita 17 na kupigiwa makofi na mashabiki.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea kucheza vizuri na kukosa mabao zaidi, huku sifa zaidi akistahili kipa chipukizi Aishi Manula.
Dakika ya 67 Telela alikarbia kufunga tena baada ya kuunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.  

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga na washindi wa pili, Azam FC kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014 kinatarajiwa kuwa Sh. 7,000.
Kiingilio hicho ni ongezeko la Sh. 2,000 kutoka kiingilio cha chini katika mchezo wa kufunga dimba la Ligi Kuu msimu uliopita, kati ya Simba na Yanga.  [[PASTING TABLES IS NOT SUPPORTED]]
Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa Ngao.
Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.
Kiingilio cha Sh. 7,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa Sh. 10,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000 na VIP A Sh. 30,000.
Wakati huo huo: Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu.
Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.
Mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani. 

BAO pekee la Gaudence Exavery Mwaikimba jioni ya leo, limeipa ushindi wa 1-0 Azam FC ya Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Mamelodi Sundwons kwenye Uwanja wa mazoezi wa timu

BAO pekee la Gaudence Exavery Mwaikimba jioni ya leo, limeipa ushindi wa 1-0 Azam FC ya Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Mamelodi Sundwons kwenye Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, uliopo Chloorkop, Johannesrbug mjini hapa.   
Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa Azam FC katika ziara yao ya nchini hapa kujiandaa na msimu baada ya juzi kufungwa mabao 3-0 na Kaizer Chiefs.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na wenyeji ndiyo waliotawala zaidi mchezo kipindi hicho, ingawa Azam walifanikiwa kutengeneza nafasi nzuri zaidi ya kufunga.

Khamis Mcha ‘Vialli’ aliingia vizuri ndani kutokea pembeni kushoto hadi ndani ya eneo la hatari na akampa pasi ya ‘hapa kwa hapa’ John Bocco ‘Adebayor’ akiwa anatazamana na lango, lakini akapiga juu ya lango dakika ya 43.   
Kipindi cha pili Azam waliingia kwa ari mpya na kufanikiwa kuuteka mchezo hali ambayo ilisababisha wafanye mashambulizi mengi langoni mwa Mamemlodi.
Almanusra Bocco afunge dakika ya 65 kama si kichwa chake kupaa juu ya lango kufuatia krosi maridadi ya Kipre Herman Tchetche.
Mamelodi walijibu shambulizi hilo dakika ya 70 na shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 19 lililopigwa na Jabu Shongwe liligonga nguzo ya juu ya lango na kurejea uwanjani kabla ya Said Morad ‘Mweda’ kuondosha kwenye hatari. 
Katika dakika ya 74, Mwaikimba aliyeingia uwanjani dakika ya 64 kumpokea Bocco aliunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya beki Joackins Atudo kutoka wingi ya kulia, ambaye pia alitokea benchi kipindi cha pili kuipatia Azam bao pekee kwenye mchezo wa leo.
Dakika ya 89 Mwaikimba alikaribia tena kufunga kama si shuti lake kupaa juu ya lango akiwa ndani ya eneo la hatari kufuatia krosi nzuri ya Tchetche.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall alifurahia matokeo na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake na pia akasifu ushindani ulioonyeshwa na wapinzani. 
Kwa wake, Pitso Masomane kocha wa Mamelodi alisifu Azam na akasema kwa soka waliyoonyesha hastaajabu kwa nini wameshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu. Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk 46, Waziri Salum/Samih Hajji Nuhu dk 80, Said Morad/David Mwantika dk77, Aggrey Morris, Jabir Azzi/Kipre Balou dk50, Himid Mao/Ibrahim Mwaipopo dk55, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk75, John Bocco/Gaudence Mwaikimbadk65, Kipre Tchetche na Khamis Mcha/Seif Abdallah dk85.
Sundown; Wayne Shandialands/Glenn dk78, Ramahlwe Mphanhlele, Punch Masenamela, Rashid Sumaila, Emanuel Mathias, Thami Sangweni/Sibusiso Khumalo dk51, Jabu Shongwe/Raymond Monama dk62, Mzikayise Mashaba, Richard Hanyekane, Elias Pelembe dk73, Surprise Moriri/Mphela Katlego dk79 na Katlego Mashego


                           AZAM YAANZA VIBAYA

AZAM FC imeanza vibaya ziara yake ya mechi za kujipima nguvu mjini hapa, baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa mazoezi wa wa timu hiyo, eneo la Nachurena.
Azam iliyoondoka nchini jana mchana kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini, kuja Johannesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya, katika mchezo wa leo iliathiriwa na uchofu wa safari na hali ya hewa ya baridi, hivyo kucheza chini ya kiwango.[[PASTING TABLES IS NOT SUPPORTED]]
Timu hiyo yenye maskani yake, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, iliyoondoka na kikosi chake kizima, kasoro wachezaji wawili tu majeruhi, kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony, imefikia katika hoteli ya Randburg Towers.
Azam jana ilifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye Uwanja wa Wits University asubuhi na jioni na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall amefurahishwa na mazingira ya kambi na Uwanja wa mazoezi.
Baada ya mchezo wa leo, Azam itashuka tena dimbani Agosti 7, kumenyana na Mamelodi Sundowns kabla ya kuivaa Orlando Pirates Agosti 9 na Agosti 12 itamaliza ziara yake kwa kumenyana na Moroka Swallows.
Azam inatarajiwa kurejea nchini Agosti 13 tayari kwa mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Safari hii Azam, washindi wa pili mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu wamepania kutwaa Ngao mbele ya Yanga, baada ya mwaka jana kufungwa na Simba SC na kocha Muingereza Stewart Hall anajiandaa kikamilifu kwa ajili hiyo.

            Sikiliza nyimbo ya Steve feat mr blue

                                 video ya leo

MASHINDANO ya vijana chini ya umri wa mika 17 ya Airtel Rising Stars 

MASHINDANO ya vijana chini ya umri wa mika 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa yamefikia tamati mwishoni mwa wiki kwa timu za Moro Kids, Alliance Schools Academy na Garden kutangazwa mabingwa katika mikoa ya Morogoro, Mwanza na Temeke.
Moro Kids imetwaa uchampioni baada ya kujikusanyia pointi nne sawa na wapinzani wao wakubwa timu ya Techfort lakini Moro Kids wakatangazwa washindi kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga. Techfort walihitimisha michuano hiyo kwa kuifunga timu dhaifu ya Anglikana 2-1 katika uwanja wa shule ya sekondari Morogoro. Magoli yao yalipatikana kupitia kwa washambuliaji Alobogast Mtalemwa na Octatus Lupekenya wakati Anglikana walifunga goli lao pekee kupitia kwa Kessy Khamis.
Hadithi ya mkoani Morogoro vile vile ilitokea huko jijini Mwanza ambapo timu ya Mwanza Alliance Schools Academy ilimemaliza ligi ikiwa na pointi nne sawa na timu ya Marsh Athletical lakini Alliance wakanyakuwa ubingwa wa mkoa kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga.
Katika mchezo wa kufunga dimba uliopigwa kwenye uwanja mkongwa wa Nyamagana Ijumaa jioni, Alliance Schools Academy na Marsh Athletical walipambana vikali katika mchezo uliovuta hisia za watazamaji wengi ambapo wachezaji wa pande zote mbili walionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kabumbu. 
Mchezo mwingine wa kufunga dimba ulipigwa katika uwanja wa Twalipo katika mkoa wa kisoka wa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo timu ya Garden wallibukwa mabingwa baada ya kuiadhibu bila huruma timu ya Mapambano 4-1. Washindi walipata magoli yao kupitia kwa Badili Salum, Bona David, Juma Masudi na Said Mohamed wakati Mapambano walipaga goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Said Hassan.
Wakati huo huo, chama cha soka mkoa wa Morogoro kimetangaza kikosi chake kitakacho uwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi Julai 7.
Kikosi chao kinajumuisha washambuliaji mapacha Evance na Robert Roshan. Wengine ni Fadhili Kamwenda, Juma Shaban, Boniface Myowela, Majid Musisi, Ramadhani Kondo, Rotan Nkamwa, Dickson Mwesa, Alphonce Lukani, Octatus Lupekenya, George Chota, Salum Kiibwa, Shafii Ngesa na Petro Mgaya.
Mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu yanashirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka mikoa tisa – Kinondoni, Ilala, na Temeke itakayoleta timu za wasichana na wavulana wakati Tanga, Kigoma na Ruvuma zitashirikisha wasichana pekee huku mikoa ya Morogoro, Mwanza na  Mbeya ikiwa na timu za wavulana tu.
Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo wa taifa yamekamilika na timu kutoka mikoani zinatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki tayari kwa mashindano hayo. Fainali za ARS Taifa vile vile zilifanyika katika uwanja huo mwaka jana ambapo Temeke waliibuka washindi.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba Juma Kaseja hakutaka kukutana na uongozi wa klabu hiyo kujadiliana juu ya mustakabali wake, licha ya kuitwa kwa miezi miwili na ndiyo maana wakaamua kuachana naye.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Poppe amesema kwamba tangu Mei wamekuwa wakimuita Kaseja kwa ajili ya mazungumzo juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo, lakini amekuwa akipiga chenga.
Poppe alisema mara ya mwisho kukutana ana kwa ana na Kaseja ni wakati wakiwa Morocco na timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mapema mwezi huu.
“Nilipokutana naye, nikamuambia sisi bado tuna nia ya kuendelea na wewe, je wewe msimamo wako ni upi? Akasema hawezi kujibu kwa sababu ana majukumu ya timu ya taifa, akimaliza atajibu. Nikamuambia sawa, wewe maliza na ukiwa tayari njoo ofisini tuzungumze.
Amemaliza mechi na Morocco, wamerudi hapa, amecheza mechi na Ivory Coast amemaliza na wiki zaidi ya mbili zimepita hajaja. Sisi tukaona huyu mtu kwa kuwa amemaliza Mkataba wake hapa na tunamuita haji, anaweza kuwa na mipango yake mingine, tumuache aendelee nayo,”alisema Poppe.
Alipoulizwa kuhusu kuachwa kwa sababu ameshuka kiwango, Poppe alisema; “Ni kweli kama utaona udakaji wake wa sasa, ameshuka mno kiwango na hilo linatupa wakati mgumu sana mbele ya mashabiki. Na kama utakumbuka Morogoro walitaka kumpiga.
Sasa ukitazama kwa mfano lile bao la kwanza alilofungwa katika mechi na Yanga, lilikuwa bao rahisi sana. Ule mpira ulipita mbele yake ukaenda kupigwa kichwa (na Didier Kavumbangu). Sasa ile kwa kweli imewaudhi sana watu,”.
“Lakini pamoja na yote, tulitaka tuzungumze naye mwenyewe, tujadiliane juu ya hali halisi, ikibidi hata kumsainisha Mkataba na kumpa fedha anazotaka, kisha tumpe mapumziko ya muda fulani, ili awe fiti arudi kazini. Lakini hakutupa fursa hiyo. Tungefanya nini?,”alihoji Hans Poppe.
Askari huyo wa zamani amesema kwamba Kaseja kama angejitambua yeye ni gwiji wa klabu, asingethubutu kupiga chenga kikao na uongozi, hususan katika kipindi hiki kigumu ambacho klabu inahitaji kujipanga upya baada ya msimu mbovu uliopita ikipoteza taji la ubingwa wa Ligi Kuu.
“Mwisho kabisa, tukaamua kumteua mtu maalumu wa kuzungumza naye, Evans Aveva. Aveva kila akimpigia simu Kaseja, anatoa udhuru, mara yuko Kigoma, mara yupo Korogwe, sasa mtu kama huyu sisi tungefanya nini?”alihoji tena Poppe.
"Na pia huyu mtu kama maslahi katika klabu hii amepata makubwa kwa sababu alikuwa anathaminiwa mno. Juma Kaseja ni kati ya wachezaji ambao watastaafu soka vizuri tu. Amevuna fedha nyingi sana hapa. Wakati wote yeye alikuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwa upande wa wazawa. Na unapofika wakati wa usajili, alikuwa anapiga hela ndefu sana hapa,"alisema Poppe. 
Historia ya Kaseja na Simba SC imefikia tamati mapema wiki hii, baada ya klabu kuamua kutomuongezea Mkataba kipa huyo iliyemsajili mwaka 2003 kutoka Moro United ya Morogoro.
Kaseja amekaririwa na gazeti la Serikali, Habari Leo akisema kwamba atawaaumbua viongozi wa Simba SC kwa kuanika kila kitu baada ya kutemwa. Lakini anapotafutwa na vyombo vingine vya habari, amekuwa akikataa kuzungumzia sakata hilo.

                              video ya leo.

Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji.

Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.
Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.
TFF KUENDESHA KOZI SITA KATI YA JULAI- SEPTEMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.
RCL KUKAMILISHA HATUA YA NNE JUMAPILI
Mechi za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.
Friends Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya. Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Hatua ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Timu ya Young Africans inatarajiwa kwenda kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki ijayo 

Timu ya Young Africans inatarajiwa kwenda kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki ijayo kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu 2013/2014, ambapo itatumia fursa hiyo kuwaonyesha  kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kusherehekea pamoja na wpenzi, washabiki na wanachama wake.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, mkurugenzi wa kampuni ya Nationwide ambao ndio waandaji wa ziara hiyo Frank Pangani amesema wao wanatumi afurs ahiyo kwa wakazi wa kanda ya ziwa kupata fursa ya kuwaona wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe lao la Ubingwa wa Vodacom pamoja na kushuhudia michezo ya kirafiki ya kimataifa.
Naye Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema ziara hiyo wataitumia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom, wanachama na wapenzi wa Yanga kuliona kombe la Ubingwa ikiwa ni pamoja na kucheza michezo ya kirafiki ambayo mwalimu ataitumia kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake.
Ziara ya Mabingwa au Champions Tour ni tukio la kila mwaka linalowahusishwa mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mabingwa wa soka waalikwa wa kutoka nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia timu alikwa ya nyumbani. 
Mara ya kwanza tukio hili lilifanyika mwaka jana 2012, kwa bingwa wa Tanzania Bara wa msimu uliopita, timu ya Simba Sports Club (SSC) ya Dar Es Salaam kushiriki ziara hiyo kucheza na mabingwa wa Uganda wa msimu uliopita timu ya The Express ya Kampala na Toto African ya Mwanza.
Mwaka jana 2012 ziara hiyo ya mabingwa ilifanyika katika mikoa ya Mwanza (Uwanja wa CCM Kirumba), Simba ilicheza na Toto African ya Mwanza, Shinyanga (Uwanja wa CCM Kambarage) Simba vs Express, na Dar Es Salaam (Uwanja wa Taifa) Yanga vs Express na Simba vs Express.
Mwaka huu 2013 itakuwa ni mara ya pili kwa tukio hili la Ziara ya Mabingwa kufanyika chini ya uandalizi wa taasisi ya michezo ya Natiowide Entertaiment Centre (NEC) yenye makao yake jijini Mwanza.
Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 itawahusisha mabingwa wa Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (YASC) ya Dar Es Salaam na waalikwa mabingwa wa mwaka huu wa Uganda timu kongwe na mashuhuri  ya Kampala City Council (KCC) ya jijini Kampala na pia timu alikwa ya ndani inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo itatangazwa ndani ya muda wa siku mbili kutoka leo.
Mechi za Ziara ya Mabingwa mwaka huu wa 2013 zitachezhwa katika mikoa ya Mwanza (CCM Kirumba) Jumamosi 06/07/2013 Yanga vs KCC, Shinyanga (CCM Kambarage) Jumapili 07/07/2013 Yanga vs KCC marudiano, na Tabora (Ali Hassan Mwinyi) Alhamisi 11/07/2013 Yanga vs timu ya nyumbani itakayotangazwa siku mbili zijazo. Baada ya mechi hizo ziara hiyo inatarajiwa kuendelea katika mikoa itakayotanagazwa baadae.
Nationwide Entertainment Centre pia inazishukuru timu zote zinazoshiriki ziara hii ya mabingwa kila mwaka wakiwemo mabingwa wa msimu huu Yanga na mabingwa wa msimu uliopita watani wao wa jadi Simba ambao wametoa ushirikiano mkubwa, na wadhamini wa mwaka huu Kilimanjaro Premium Lager na vyombo vya habari.
Source: http://youngafricans.co.tz